simplebooklet thumbnail

reducing child mortality rates by creating awareness on how to deal with basic emergency conditions before reaching the health center

of 0
MWONGOZO WA KUPUNGUZA UKALI WA DHARURA NA SUMU KWA WATOTO
KABLA YA KUFIKA HOSPITALI
KUMMUDU MTOTO ALIE PALIWA (CHINI YA MWAKA 1)
Mlaze motto mkononi au pajani mwako, kichwa chake kikitizama chini.
Gonga mara 5 na kiganja cha mkono wako katikati ya mgongo wake
Kama bado mtoto amepaliwa, mgeuze upande wa pili, tumbo likitizama juu na
kichwa kikitizama chini kidogo, gonga mara tano kifuani (nusu ya chini ya kifua)
kwa kutumia vidole vyako viwili
Kama bado mtoto anapaliwa, tizama mdomoni kama kuna kitu kinachomziba
ambacho kinaonekana kwa macho yako tu.
Kama bado rudia kumgonga mgongoni mara tano
Muwahishe katika kituo cha karibu cha afya
KWA MTOTO ZAIDI YA MWAKA 1
Gonga mara 5 na kiganja cha mkono wako katikati ya mgongo wake mtoto
akiwa amelala chali au amepiga magoti au amekaa.
Kama bado amepaliwa, nenda nyuma ya mtoto na zungusha mikono yako kwa
mtoto juu ya eneo la tumbo, ukiwa umekunja ngumi kwa mkono mmoja na
mkono wa pili kushikilia ngumi ya mkono wa kwanza, vuta ndani (kuelekea
ndani ya tumbo kwa nguvu hadi mara tano.
Kama bado mtoto anapaliwa, tizama mdomoni kama kuna kitu kinachomziba
ambacho kinaonekana kwa macho yako tu.
Kama bado rudia kumgonga mgongoni mara tano
Muwahishe katika kituo cha karibu cha afya
KUMMUDU MTOTO ALIEACHA KUHEMA GHAFLA
KAMA MTOTO HAJAUMIA/KUJIGONGA SHINGO
KAMA MTOTO YUPO MACHO
Fungua mdomo na toa kitu chochote kinachoonekana kwa macho tu
kinachoziba hewa. Pia tizama puani kama kunachochote kinachoziba. Mf.
Harage, njegere, jiwe n.k
Kausha matemate ya mdomoni na kitambaa
Mtoto alale anavoona yeye atapata hewa ya kutosha
Mkimbize hospitali
KAMA MTOTO AMEZIMIA
Inamisha shingo ya mtoto kama kwenye picha hii na nyanyua kidevu chake
kufungua njia ya hewa
Fungua mdomo na toa kitu chochote kinachoonekana kwa macho tu
kinachoziba hewa. Pia tizama puani kama kunachochote kinachoziba. Mf.
Harage, njegere, jiwe n.k
Kausha matemate ya mdomoni na kitambaa
Mkimbize hospitali
KAMA MTOTO AMEACHA KUHEMA NA AMEUMIA SHINGO
Funga kidevu na utosi wa kichwa wa mtoto kwenye ubao mgumu au kitu
chochote kigumu ili kupunguza kucheza kwa shingo au kichwa. Unaweza
kutumia nguo kuweka kila upande wa kichwa utakapo fungia na kamba ili
kupunguza kuchezesha kichwa
Fungua mdomo na toa kitu chochote kinachoonekana kwa macho tu
kinachoziba hewa. Pia tizama puani kama kunachochote kinachoziba. Mf.
Harage, njegere, jiwe n.k
Kausha matemate ya mdomoni na kitambaa
Mkimbize hospitali
Kama mtoto anatapika mgeuze kiupande, ila kichwa kiwe usawa mmoja na
mwili, usikitingishe wala shingo.
MTOTO ALIEATHIRIKA NA SUMU
MKIMBIZE MTOTO KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KARIBU KWANI SUMU
HUWEZA ATHIRI VIUNGO VYA MWILI, KUINGILIA NJIA ZA HEWA, KUPUNGUA
KWA DAMU AU KUZIMIA.
HUTAKIWI KUMTAPISHA MTOTO KAMA:
Mtoto amezimia
Mtoto amemeza au kunywa sumu za petrol (dawa za kuua wadudu na
kupulizia mimea nyingi huwa bidhaa za petrol)
Mdomo wa mtoto umeungua mdomo na kinywa (sumu nyingi zinazoweza
sababisha hii hali ni kama jiki, dawa za kuoshea choo au maji ya battery)
SUMU KWENYE NGOZI
Vua nguo na toa vifaa vyote vilivoshikamana na hio sumu au kemikali
Osha mara nyingi na maji yaendayo kwa kasi
Tumia sabuni pia kama sumu ni ya asili ya mafuta
Wahi katika kituo cha karibu cha afya
SUMU MACHONI
Osha jicho kwa dakika 10-15 kwa maji masafi. Hakikisha mwelekeo maji sio
kuelekea katika jicho lingine ili lisipate sumu pia.
Wahi katika kituo cha karibu cha afya
SUMU KATIKA NJIA YA HEWA
Mtoe mtoto katika chanzo hiko cha sumu
Mkimbize katika kituo cha karibu cha afya
Mpe mtoto hewa ya kutosha mkielekea katika kituo cha afya
SUMU ZA KUUNGUZA
Usimtapishe mtoto kama amekunywa sumu hizi
Mpe maji au maziwa kama yapo yapunguze makali ya sumu hizi
Mkimbize katika kituo cha karibu cha afya
MTOTO ALIYEMEZA PANADOL AU ASPIRIN NYINGI
Kama ndani ya masaa manne mtapishe
Mkimbize katika kituo cha karibu cha afya
WAZAZI TAHADHARI!!! WEKA CHUPA NA MAKASHA YA MADAWA NA SUMU
ZINGINE MBALI NA WATOTO.